The House of Favourite Newspapers

Pwani: Jamii ya Wafugaji na Wakulima Yakumbwa na Baa la Njaa

ukame91PWANI: Jamii ya wafugaji na wamkulima wa vijiji vya Gumba, Chaua na Gwata mkoani Pwani imekumbwa na baa la njaa kutokana na ukame kwa kukosa mvua mito kukauka na mifugo yao ikifa kwa kukosa chakula na maji.

Ukame huo unatajwa kuvikumba viviji hivyo tangu mwaka jana mwezi wa pili na kukosa mvua msimu mzima ambapo baadhi ya wananchi wakulima na wafugaji akiwemo mwenyekiti wa kijiji cha Chaua wanazungumzia hali hiyo kuwa inahitaji msaada wa haraka kunusuru maisha yao.

Aidha baadhi ya wafugaji wa vijiji hivyo wanaeleza kipindi hicho mamia ya mifugo yao kufa kwa kukosa maji na kubainisha njia mbadala ya kutumia visima vya kuchimba chini ya ardhi ili kuzuia vifo hivyo ambavyo vinaendelea kuongezeka siku hadi siku huku mbunge wa jimbo hilo la Chalinze Ridhiwan Kikwete akikiri hali hiyo akieeleza jitihada zake za kuomba msaada wa chakula ili kunusuru jamii hiyo.

Aizungumzia hali hiyo kwa njia ya simu mkurugenzi wa hamlashauri ya Chalinze mkoani Pwani Bw. Hades Lukoa pamoja na kukiri hali hiyo ameeleza kuwa tayari wizara ya kilimo imetuma timu ya wataalamu ambayo imeanza kazi ya kuchambua athali na hali halisi ya ukame na kwamba watatoa taarifa mishoni mwa wiki.

CHANZO: ITV

Comments are closed.