The House of Favourite Newspapers

Queen Darleen: Nungunungu au Karunguyeye?

0

Mwimbaji Queen Darleen anasema ameshindwa kujipa jina la mnyama kutokana yale makubwa na yanayosifika yameshachukuliwa na kama kutakuwa na ulazima wa yeye kufanya hivyo, basi atatumia jina la Nungunungu au Karunguyeye.

 

“Unajua kila anachofanya msanii ana lengo lake, kuna shabiki muda mwigine hajisikii kukuita Queen Darleen, anataka tu kukuita Nungunungu, kwa hiyo inaleta ladha fulani,” amesema Darleen.

 

Baadhi ya wasanii wanaotumia majina ya wakali ni Diamond Platnumz (Simba), Harmonize (Tembo), Rayvannny (Chui), Country (Fisi), Dubu Baya (Mamba) na Afande Sele (Simba).

Leave A Reply