The House of Favourite Newspapers

SGA Security Yazindua Kituo cha Kisasa cha Mawasiliano

0
Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania, Eric Sambu (wa tatu kutoka kulia) akiwaongoza baadhi ya wafanyakazi kukata keki kama ishara ya uzinduzi wa kituo cha kisasa cha mwawasiliano wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Fedha, Jonathan Geleta, Meneja Huduma za Ulinzi, Joakim Sabana , Meneja Rasilimali Watu Ebenezer Kaale, Meneja Huduma kwa Wateja, Aikande Makere na Meneja Ufundi, Prochest Peter.

 

 

 

SGA Security, ambayo ni moja ya makampuni yanayoongoza katika huduma za ulinzi, imezindua kituo cha kisasa cha mawasiliano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, uliofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo, Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania, Eric Sambu alisema kituo hicho kipya kitatoa huduma saa 24 na ni otomatiki.

Meneja wa Kituo Cha Mawasiliano wa SGA Security Joseph Mushi (kulia) akitangaza namba itakayotumiwa na wateja kuwasiliana na kituo cha mawasiliano cha kampuni hiyo wakati wa uzinduzi wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Tanzania, Eric Sambu.

 

 

 

Alisema kampuni hiyo inajivunia katika kutoa huduma bora na za viwango vya juu kwa sababu imewekeza katika mitambo ya kisasa na mafunzo kwa wafanyakazi na yote haya yatakuwa na ufanisi ikiwa mawasiiano kati ya kampuni na wateja yatafanyika kwa haraka zaidi.

Uongozi wa Kampuni ya SGA Tanzania katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa kituo hicho ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

 

 

 

“Tuna imani na wafanyakazi wetu  na tumewekeza vilivyo katika kuwawezesha ili waiwakilishe kampuni vizuri kwa fahari. Tunaamini kituo hiki kitasababisha wafanye kazi kwa weledi zaidi na kwa kujiamini,” alisema.

 

 

Alisema timu za dharura za SGA zina mawasiliano ya moja kwa moja na chumba cha mawasiliano mara tu inapobonyezwa alarm na wafanyakazi wa kituo cha mawasiliano wanaweza kuona maeneo walipo kwa kutumia mitambo maalumu iliyounganishwa kwenye ramani za google na kuweza kuwaongoza katika eneo liliporipotiwa tukio. Ishara fulani huonekana kwenye ramani kwani gari liliklokokaribu pia hupewa taarifa kuwahi katika eneo la tukio.

 

 

“Nguvu yetu ipo katika uwezo wa timu zetu kuwahi katika eneo la tukio huku wakiwa na vifaa vya kutosha, mafunzo na silaha,” alisema Bw. Sambu. Meneja Huduma kwa Wateja wa SGA Tanzania, Aikande Makere alisema wateja wategemee huduma bora zaidi baada ya uzinduzi wa kituo hicho cha kisasa.

 

 

“Tutaweza kufuatilia matukio kwa karibu zaidi kwa kupitia mfumo huu mpya,” alisema na kuongeza kituo hicho kitatoa huduma saa 24 na kwamba kuna wafanyakazi sita katika kila zamu huku wakipeana muda wa kupumzika ili kuhakikisha hawapati uchovu.

 

 

“Kwetu sisi mteja ni muhimu na tutafanya kila jitihada kuhakikisha tunaepusha malalamiko miongoni mwa wateja,” alisema. Naye Meneja Masoko wa SGA Tanzania, Faustina Shoo, alisema kampuni hiyo itatoa punguzo la asilimia 25 kwa bei ya huduma za dharura kwa miezi mitatu ijayo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

 

 

Alisema lengo la SGA sio kufanya tu biashara bali kuisaidia serikali katika kuhakikisha kuna amani na utulivu ili wananchi waweze kufanya biashara na shughuli nyingine kwa amani. “Tunataka kuhakikisha wateja wetu wanaendelea na shughuli zao bila kuwa na uoga huku wakiwa na uhakika kuwa SGA ipo katika kuwalinda wao na mali zao,” alisema.

 

 

Mwaka jana kampuni hiyo ilipokea tuzo baada ya kutangazwa mshindi wa jumla kama kampuni yenye rasilimali za kutosha na ya kuaminika  (Most Equipped and Reliable Security Company of the Year, 2020) katika tuzo za chaguo la wateja (Consumer Choice Award).

 

 

SGA Security inatoa huduma mbalimbali ikiwemo za ulinzi, alarm, huduma za fedha, ulinzi wa kielektroniki, huduma ya kusafirisha mizigo na huduma nyinginezo na  ndio kampuni pekee ya ulinzi yenye cheti cha ISO 18788 – Security Operations Management System-kiwango cha dhahabu. Hii ni pamoja na vyeti vingine viwili vya ISO 9001 na ISO 45001

Leave A Reply