The House of Favourite Newspapers

Bongo Fleva: Quick Rocka Kuachia Wimbo Na ‘Mimi Mars’ – Mdogo Wake Vanessa Mdee!

Mara ya mwisho kumsikia Quick Rocka kwenye anga za burudani ilikuwa kwenye ngoma yake ya mwisho ya Mwendokasi, wimbo aliyomshirikisha rappa mwengine wa Bongo Fleva, Chin Bees. Team ya Global Publishers ikaamua imtafute rappa huyo na kumuuliza mipango yake ya kimuziki kwa mwaka huu wa 2017 ipoje.

Kwenye Exclusive interview na Global Publishers, Quick Rocka ameelezea mipango hiyo na kusema kuwa mwezi huu anategemea kuachia ngoma mpya itakaomshirikisha mdogo wake Vanessa Mdee, Marianne Mdee maarufu kama ‘Mimi Mars’. Akaendelea kusema kuwa msichana huyo ni mmoja kati ya wasanii wakali wa kuwaangalia kwa mwaka huu.

 

Marianne Mdee – Mimi Mvrs

>>”Mimi Mars ni mdogo wake Vanessa Mdee na nathubutu kusema ni msanii wa kumuangalia sana kwa mwaka huu, she’s a bomb. Ni msanii wa kike ambaye anakuja na atakuwa noma…“<< – Quick Rocka.

Vipi? Kichupa cha video na audio tukitegemee lini?

>> “Ujio wa Quick Rocka na Mimi Mars, video na audio ni end of this month… ngoma ni KALII!!“<< – Quick Rocka.

 

Comments are closed.