The House of Favourite Newspapers

Mo Music: Skendo Zinamuumiza Baba’ngu

Na GABRIEL NG`OSHA| RISASI MCHANGANYIKO| HABARI/ BURUDANI

MSANII wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ amefunguka kuwa anaogopa kukumbwa na skendo kwa vile jambo hilo likitokea, baba yake hupatwa na shinikizo la damu, kitu ambacho ni hatari.

Akizungumza na Risasi Vibes, Mo Music alisema hapendi mambo ya skendo kwa sababu anampenda na kumheshimu baba yake, maana kila anapoona jambo hilo kwenye vyombo vya habari hupandwa napresha kulazwa hosptiali nampenda sana baba yangu na ninaijali familia yangu lakini ishu ya skendo mara nyingi zimekuwa zikimuweka kwenye wakati mgumu baba yangu, huamsha maradhi ya moyo (presha) na kuwa shida, ndiyo maana nimekuwa nikizikwepa sana ili zisinitokee zikaleta matatizo,” alisema Mo Music.

Comments are closed.