The House of Favourite Newspapers

Maofisa Upelelezi Kortini kwa Tuhuma za Rushwa

MAOFISA wa upelelezi wanne wa kituo cha Polisi Kawe wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka tisa likiwemo la kuomba rushwa ya Sh. 200 milioni na kupokea rushwa zaidi ya Sh 15 milioni.

 

Upande wa mashtaka umedai kati ya washtakiwa hao, mshtakiwa namba mbili, Emmanuel Njegele, hakuwepo mahakamani,  hapo hivyo, wameomba hati ya kukamatwa kwake. Washtakiwa wengine ni Shaban Shillah, Joyce Kitta na Ulimwengu Rashid.

 

Akisoma hati ya mashtaka Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Maghela Ndimbo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile amedai kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na kosa la kushawishi na kupokea rushwa, kugushi nyaraka za uongo na kutotii amri halali ya ofisa wa Takukuru.

 

Wakili Ndimbo amedai kuwa kosa la kwanza la ni la rushwa ambapo washtakiwa wote kwa pamoja wanadaiwa walitenda kosa hilo Desemba 17, 2018 eneo la Social Club Rainbow Kinondoni wakiwa maofisa wa upelelezi walishawishi rushwa ya sh. 200 milioni kutoka kwa Diana Naivasha wakidai amekamatwa na Nyara za Serikali ili kushawishi hatua za kisheria zisichukuliwe dhidi yake.

 

Kosa jingine nila kupokea rushwa ambapo kwa pamoja wanadaiwa Desemba 17, 2019 katika Kituo cha Polisi cha Kawe jijini Dar es Salaam waliomba rushwa ya Shiling million 6 kutoka kwa Diana Naivasha kama kishawishi cha kumsaidia asichukuliwe hatua za kisheria baada ya kukamatwa na nyara za Serikali.

 

Katika kosa la nne, tano na sita ni kujihusisha na rushwa ambapo inadaiwa walilitenda kosa hilo Desemba 19, 2018 , Desemba 23, 2018, Januari 3, 2019 washtakiwa hao wakiwa Kituo cha Polisi cha Kawe, kama waajiriwa katika nafasi zao walipokea sh 2 milioni kutoka kwa Diana Naivasha kama kishawishi cha rushwa kwa madai anajihusika na nyara za Serikali.

 

Kosa jingine nila kughushi nyaraka linalomkabili Joyce Kitta ambapo anadaiwa alitenda kosa hilo Desemba 2018 na Aprili 3, 2019 katika maeneo ya Kinondoni akiwa kama mwajiriwa wa Polisi kwa lengo la kudanganya alitengeneza nyaraka za uongo kwa jina la Diana Thomas Naivasha akidai nyaraka hizo ni za kweli na zimewekwa sahihi na Diana wakati akijua si kweli.

 

Pia katika kosa la mwisho la kutotii amri halali ya Ofisa wa Uchunguzi wa Takukuru ambapo inadaiwa Aprili 2019 wakiwa eneo la baa Kinondoni wakiwa waajiriwa wa Polisi kwa pamoja walishindwa kutii amri halali ya kukamatwa ambayo ilitolewa na Mpelelezi wa Takukuru, Colman Lubisi.

 

Baada ya kusomewa mashitaka hayo washitakiwa walikana makosa yao ambapo Wakili Ndimbo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia hawana pingamizi na dhamana. Hakimu Rwizile ametoa masharti ya dhamana hiyo ambapo wanatakiwa kusaini bondi ya Sh 10 milioni kwa kila mmoja pamoja na wawasilishe hati za kusafiria mahakamani.

 

Hata hivyo washtakiwa hao wameshindwa kutimiza masharti hayo isipokuwa mshtakiwa Shillah,  na Kesi hiyo meahirishwa hadi Oktoba 16,2019. Awali kabla ya kesi hiyo kuanza mshtakiwa namba moja Shaban Ramadhaan Shillah alionekana akitoa lugha ya vitisho kwa waandishi wa habari waliokuwa wakipiga picha.

Comments are closed.