The House of Favourite Newspapers

Rage: Msimu Huu Simba Wanakwenda Kubeba Kila Kitu, Atamba na Usajili wa Mserbia

0

BAADA ya uongozi wa Simba kukamilisha usajili wa straika Mserbia, Dejan Georgijevic, mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo, Ismail Rage, amefunguka kuwa, msimu huu wanakwenda kurudisha mataji yote waliyopoteza msimu uliopita.

 

Simba imeendelea kujiimarisha kwenye eneo lake la ushambuliaji ambapo msimu huu wamekamilisha usajili wa viungo washambuliaji Nelson Okwa, Moses Phiri, Augustine Okrah na straika Dejan Georgijevic.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Rage alifunguka kwamba: “Msimu uliopita haukuwa bora upande wetu, hii ilitokana na aina ya usajili ambao tulifanya, wachezaji wengi walishindwa kutupa kile ambacho tulitarajia huku wengine wakiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

“Msimu huu viongozi wetu wamejua wapi tuliteleza na aina ya usajili uliofanywa ni wazi tunakwenda kuwa tishio.

 

“Wachezaji waliosajiliwa msimu huu wote ni wazuri na nina uhakika tunakwenda kurudisha makombe yetu yote ambayo watani zetu Yanga wameyatwaa msimu uliopita, wachezaji wanapaswa kutambua kuwa wana deni kubwa kwa mashabiki, hivyo wanatakiwa kupambana katika mechi zote watakazocheza iwe nyumbani au kimataifa.”

 

Usajili wa Mserbia huyo unatajwa kuwa ni pendekezo la kocha Zoran Maki ambaye amemshusha mwamba huyo kama mbadala wa Chris Mugalu aliyesitishiwa mkataba wake kutokana na kutokuwa na mwenendo mzuri ukichangiwa na majeraha ya mara kwa mara.

STORI: HUSSEIN MSOLEKA

CAF YAZIPELEKA SIMBA, YANGA UGENINI, NABI ASHTUKA FASTA AISUKA SAFU YA ULINZI YANGA | KROSI

Leave A Reply