The House of Favourite Newspapers

Raila Odinga ‘Father Christmas’

0

Kiongozi wa Chama cha Orange Democratic MovementiODM‘ nchini Kenya, Raila Odinga amesheherekea sikukuu ya Christmas kwa kutoa misaada mbalimbali kwa watoto wenye uhitaji.

Waziri mkuu huyo wa zamani wa Kenya amewavutia maelfu ya watumiaji wa mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa picha kadhaa zikimuonesha akiwa katika hafla hiyo fupi akigawa zawadi kwa watoto huku akiwa amevalia mavazi ya ‘Father Christmas’.

Katika hotuba fupi aliyoitoa, Odinga aliwatakia watoto Krismasi njema na mwaka mpya wa 2022 wenye mafanikio, na kuwataka wawe waangalifu katika kipindi hiki cha sikukuu ili kuepuka kuambukizwa Covid-19.⁣

Leave A Reply