The House of Favourite Newspapers

Raila Odinga: Hatufanyi Maongezi Tena Na Ruto, Lazima Tumzuie Sasa

0
Kiongozi huyo wa Muungano wa Vyama vya Upinzani kupitia Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga.

Kiongozi huyo wa Muungano wa Vyama vya Upinzani kupitia Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga amesema wamefuta mazungumzo yote na Serikali baada ya Rais William Ruto kusaini Sheria ya Fedha

Amesema wanarejea katika kampeni za kuhamasisha migomo ya Wananchi dhidi ya jambo lolote la Serikali ikiwemo kutolipa Kodi zote ili kushinikiza Ruto aondoke Madarakani

Odinga ameongeza “Ruto anajaribu kuona kama tuna nia, nguvu na azimio la kupigana na udikteta. Tunapaswa kumzuia Ruto na tunapaswa kufanya hivyo sasa.”

MUSUKUMA AWACHANA SIMBA “WANASAJILI MAKAPI, MPIRA NI PESA SIO SWAGA MPIRA UNAHITAJI PESA”

Leave A Reply