The House of Favourite Newspapers

Video: Aliyekuwa Mpigapicha Wa Jux Amwaga Shombo Kwa Bosi Wake, Adai Makabila Kamchukulia Mke…

0

Kupitia kipindi cha Mapito kinachoruka hewani kupitia 255global radio, mpiga picha wa zamani wa msanii wa Bongofleva Jux, @mingoclass amekanusha kuhusu tetesi zilizokuwa zikivuma kwamba amefukuzwa kazi na bosi wake huyo wa zamani, Jux.

Katika maelezo yake @mingoclass ameeleza kwamba hakuna ukweli wowote kwamba yeye amefukuzwa kazi na Jux na badala yake yalikuwa ni makubaliano yao binafsi.

@mingoclass ameeleza kwamba ilifika wakati akatamani kufanya kitu kizuri Zaidi ya kupiga picha hivyo alimfuata Jux na kuzungumza naye ili kumuomba amruhusu akaanze maisha yake ya kimuziki na ndipo walipofikia makubaliano ambapo Jux alikubali kumruhusu, hivyo hakuna ukweli wowote ule kwamba alifukuzwa kazi na Jux.

“Kama niliweza kuacha kazi kwa msanii mkubwa kama Jux, basi siwezi kuwa mpiga picha wa huyo msanii unaye mtaje, hana thamani ya mimi kuwa mpiga picha wake” anasema Mingo Class

Leave A Reply