The House of Favourite Newspapers

Rais Aongoza mazishi Ya aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa Mkoani Arusha (Picha +Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiweka udongo kwenye kaburi la Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema, miongoni mwa vitu alivyojifunza kutoka kwa hayati Edward Ngoyai Lowassa ni kiongozi ambaye ukimheshimu anakuheshimu pia.

“Nilijifunza mengi kutoka kwake (hayati Edward Ngoyai Lowassa). Kati ya hayo, nililoliona kwa mheshimiwa Lowassa ni kwamba ukimheshimu, anakuheshimu.”

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Februari 17, 2024 wakati akitoa neno la pole kwa familia ya aliyekuwa Lowassa wakati wa maziko yake kijijini kwake Ngaresh wilayani Monduli mkoani Arusha.

Pamoja nna hilo,Rais Samia amesema Lowassa hakuwahi kuwasema vibaya wapinzani wake wa kisiasa pindi alipoamua kuhama chama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongoza viongozi mbalimbali wakati wa mazishi wa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa leo Februari 17, 2024  Mkoani Arusha.

Rais Samia akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa Marehemu Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.

Rais Samia akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Waombolezaji wakati wa Shughuli za Mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa katika Kijiji cha Ngarash, Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji Mama Regina Lowassa Mjane wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa mara baada ya shuguli za Mazishi zilizofanyika Nyumbani kwa Marehemu Ngarash, Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.

 

Leave A Reply