The House of Favourite Newspapers

Rais George Weah Amtunuku Tuzo ya Juu Kocha Arsène Wenger

RAIS wa Liberia, George Tawlon Manneh Oppong Ousman Weah ‘George Weah’ amemtunuku aliyekuwa Meneja wa Klabu ya Arsenal, Arsène Wenger, Tuzo ya Hadhi ya Juu Zaidi The Knight Grand Commander of the Humane Order of African Redemption’ nchini Liberia kwenye sherehe iliyoandaliwa kwenye Mji Mkuu, Monrovia.

Wenger alikuwa kocha wa kwanza wa Rais George Weah kwenye klabu ya Ulaya baada ya Wenger kumsajili kuitumikia Monaco 1988.

 

Weah (51) ndiye Mwafrika wa kwanza kushinda Tuzo ya Fifa la Mchezaji Bora wa Mwaka aliyoinyakua mwaka 1995. Alistaafu kutoka soka mwaka 2003 na kuingia siasa.

Hatua ya Wenger kutuzwa hatua hiyo imezua maoni tofauti nchini humo huku baadhi wakisema kuwa tuzo hiyo haistahili kupewa mtu binafsi kwa kile amemfanyia rais pekee.

 

Lakini tuzo hiyo si tuzo kuhusu uhusiano wa Rais na Wenger bali inatambua kile Wenger amechangia kwa michezo Barani Afrika na kuwapa Waafrika wengi fursa katika timu alizozinoa Mfaransa huyo.

Rais Weah amesema kuwa Wenger “alinitunza kama mtoto wake” wakati alijiunga na Monaco, akisema kuwa “kando na Mungu, anafikiri kuwa bila ya Wenger hakuna vile nigefanikiwa Ulaya”.

Comments are closed.