The House of Favourite Newspapers

Rais Jela Miaka 12 kwa Ufisadi

MAHAKAMA ya Rufaa nchini Brazil imeagiza kuwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva ni sharti aanze kutumikia kifungo chake cha miaka 12 gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na ufisadi.

 

Majaji sita kati ya 11 wa mahakama hiyo walipinga rufaa hiyo huku watano kati yao wakimuunga mkono. na kesi hiyo kusababisha hali ya wasiwasi wa kisiasa nchini humo.

 

Hatia hiyo imetokana na uchunguzi wa muda mrefu wa sakata la rushwa linalojulikana kama ”Operation Car Wash” ambapo Lula alibainika kukubali rushwa ya thamani Euro 790,000.

 

Lula da Silva amekua akitarajiwa na watu wengi kusimama kama mgombea asiye na ushindani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba, lakini ndoto hizo zimeyeyuka baada ya mahakama kuamuru mwanasiasa huyo mkongwe aanze kifungo chake.

 

Maandamano yamefanyika katika miji mbalimbali, waandamanaji katika mji wa Sao Bernardo wanataka Da Silva aachiwe huru huku baadhi ya watu wakipinga kuachiwa kwake huru na badala yake jeshi ndio liongoze nchi hiyo.

 

Mbali na kukutwa na hatia, Lula amekua akipinga vikali kuhusika na kashfa yoyote ya rushwa anasema kuwa amekua akipinga vikali uonevu wa aina yoyote hivyo hatakubali uonevu wa mahakama.

 

Kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 72 atabaki uraiani kwa muda hadi pale nyaraka za kifungo chake zitakapo kamilika. Da silva amekua madaraki kati ya mwaka 2003 hadi 2011. Iwapo angeingia kama mgombea katika uchaguzi wa mwezi Oktoba huenda angeshinda kwa kishindo kutokana na umaarufu wake.

 

Nondo Aitwa Kuhojiwa Kuhusu Uraia Wake

Comments are closed.