The House of Favourite Newspapers

Rais Joe Biden kutembelea Israel na Jordan wiki hii kuzungumzia hali ya vita vya Gaza

0
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken, ametangaza Jumanne kwamba Rais Joe Biden atatembelea Israel siku ya Jumatano kufuatia mashambulio ya Hamas, na ametangaza kwamba Israel imekubali kufanya kazi na Marekani na Umoja wa Mataifa kuwasilisha msaada kwa wakazi wa Gaza.

Blinken alitoa tangazo hilo baada ya kuwa na mazungumzo ya karibu saa nane na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, kwenye wizara ya Ulinzi ya Israel, akiwa katika ziara yake ya pili ya nchi hiyo tangu Oktoba 7 pale Hamas iliposhambulia Israel.

Blinken alisema mjini Tel Aviv, kwamba Rais Biden atathibitisha tena ungaji mkono wa Marekani kwa Israel na kueleza dhamira zake za dhati kwa ajili ya usalama wa taifa hilo.

Kwa upande mwengine, Blinken anasema Marekani imepata uhakikisho kutoka kwa Israel juu ya kutayarisha mpango wa kuruhusu msaada wa kigeni kuingia katika kanda iliyozingirwa na yenye hali duni ya Gaza, wakati Israel inajitayarisha kwa uvamizi wa nchi kavu dhidi ya maeneo yanayoshikiliwa na Hamas.

Mwanadiplomasia mkuu wa marekani yuko katika siku yake ya tano ya mazungumzo mfululizo na viongozi wa nchi za Mashariki ya Kati, katika juuhudi za kutafuta suluhisho kwa mzozo wa Gaza kati ya Israel na Hamas.

Wakari huo huo, msemaji wa Baraza la Usalama wa Taifa la Marekani, John Kirby alitangaza mjini Washington Jumatano, kwamba Biden atatembelea pia Jordan ambako atakutana na Mfalme Abdullah wa Pili, Rais Mahamoud Abass wa Palestina, na rais abdel Fatah al Sisis wa Misri.

Kirby aliwambia waandishi9 habari kwamba Rais Biden atasisitiza tena kwamba Hamas haiwakilishi maslahi ya Wapalestina ya haki yao ya kupata utawala wao, na atazungumzia pia msaada wa dharura kwa rais wa Gaza.

Leave A Reply