The House of Favourite Newspapers

Vifo vya Mashabiki Wawili wa Sweden Vyapelekea Mechi Kuahirishwa

0

Mchezo wa kufuzu EURO 2024 kati ya Ubelgiji na Sweden umeahirishwa baada ya wachezaji kugoma kurudi uwanjani kipindi cha pili kutokana na vifo vya mashabiki wawili wa Sweden waliopigwa risasi katika shambulio la kigaidi mjini Brussels kabla ya mchezo huo.

Mamlaka ya soka ilitakiwa kuufuta mchezo lakini haikufanya hivyo wachezaji wameamua kugoma kurudi Uwanjani.

Mashabiki wa soka wametakiwa kusalia ndani ya uwanja wa taifa wa Ubelgiji kufuatia shambulio hilo.

Mpaka mechi inaahirishwa matokeo yalikuwa 1-1 mpaka mapumziko.

HT: Ubelgiji 🇧🇪1-1 🇸🇪 Sweden

Leave A Reply