The House of Favourite Newspapers

RAIS JPM AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA MAMA YAKE SHIGONGO

BADO huzuni, vilio na majonzi vimetanda kwenye familia ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Group, Eric Shigongo, baada ya kuondokewa na mama yao mpendwa Bi. Asteria Kapela aliyefariki Ijumaa iliyopita, katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar.

Hata hivyo katika kuomboleza msiba huo, familia ya Shigongo imeshirikiana na watu mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wake, majirani, jamaa, marafiki na viongozi mbalimbali wa nchi. Viongozi wa nchi waliopata nafasi ya kuifariji familia ya Shigongo, waliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ‘JPM’, mkewe Bi Janeth Magufuli pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Watu wengine maarufu waliopata nafasi ya kufika nyumbani kwa marehemu Mikocheni B, kuifariji familia ya Shigongo ni pamoja na Dkt. Mwigulu Nchemba, Nape Nauye, Jerry Muro, Asha Baraka, Masanja Mkandamizaji, Faidha Omary ‘Sister Fay’ pamoja na wengine wengi. Mwili wa marehemu Bi Asteria uliagwa Jumapili iliyopita nyumbani kwake Mikocheni kisha kufanyiwa misa kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Martha lililopo Mikocheni.

Baada ya hapo safari ya kuelekea nyumbani kwake jijini Mwanza ilianza ambako mwili wake uliagwa nyumbani kwake jana Nyakato Mecco kisha kusafirishwa tena kwenda katika Kijiji cha Bupandwamhela, Buchosa wilayani Sengerema kwa ajili ya kupumzishwa katika nyumba yake ya milele kesho Jumatano.

BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.