The House of Favourite Newspapers

JPM Awaambia Wapiga Kura: Hamchagui Malaika – Video

0

MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, (CCM), Dkt. John Magufuli, amesema kuwa anatamani taifa la Tanzania liendelee kuheshimika zaidi duniani na kwamba anatamani siku moja Tanzania iingie uchumi wa kwanza.

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 26, 2020, wakati akizungumza na wananchi wa Dodoma, ikiwa ni mwendelezo wa mikutano yake ya kampeni kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika  Jumatano ya Oktoba, 28 mwaka huu.

 

Awali Dkt Magufuli akiwa katika jimbo la Kondoa akiomba kura alisema: “Hamchagui malaika, mnachagua binadamu, ninawaomba ndugu zangu ili mnisaidie kupata ‘connection’ ya kazi, nipate watu watakaokuja ofisini waniambie CCM oyee!”

 

Akifafanua zaidi mambo atakayofanya, aliendelea kusema kwamba: “Mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima gharama yake Tsh trilioni 8 na utatoa ajira za watu zaidi ya elfu 15 achilia, mbali mama lishe na wengine. Niwaombe wawekezaji wengine waje Tanzania. Tunahitaji wawekezaji kama Total, Barrick ambao walikubali kukaa chini tukakubalina.

 

“Mkinichagua nitafanya makubwa. Nitashangaa sana maana nimeacha maeneo mengi, makao makuu sikupeleka kwingine nikaleta hapa Chamwino halafu msinipe kura!   Unajua Wagogo watani zangu saa nyingine hamuaminiki. Naomba mnipe kura.

 

“Leo nipo kwenye jimbo ambalo ninakaa, Jimbo la Chamwino nimetokea Manyara. Makaribisho haya yanaonyesha kwa kweli mwaka huu mnafanya maajabu. Hapa usafiri ulikuwa wa shida, leo maisha yamebadilika. Utakuta mtu anasema kujenga barabara sio kitu, hajui ni watu wangapi waliokufa kwa kushindwa kufika hospitalini kwa sababu barabara ni mbovu na daraja kuvunjika,” amesema Magufuli.

 

Leave A Reply