The House of Favourite Newspapers

Rais Kenyatta Azindua Kiwanda cha Bunduki

0

Rais Uhuru Kenyatta amezindua kiwanda cha utengenezaji bunduki ambacho ni sehemu ya viwanda vya vifaa vya usalama wa kitaifa eneo la Ruiru Kaunti ya Kiambu, Kenya.

 

 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kenyatta amesema kiwanda hicho kitasaidia katika kuimarisha uchumi wa kitaifa na ufanisi wa kiteknolojia Kenya.

 

“Kiwanda hiki kitasaidia Sekta ya Usalama kuwa huru, pia tutaimarisha uchumi na kupunguza gharama ya kununua silaha nje ya nchi,” amesema Kenyatta.

 

 

Amesema kiwanda hicho pia kitapunguza gharama ya ununuzi wa silaha nje ya Nchi (kwa hadi 60%) na kuwezesha sekta ya usalama kuwa huru huku akisema Kenya itaendelea kuimairisha utengenezaji wa vifaa vya kisasa vya usalama.

Leave A Reply