The House of Favourite Newspapers

RAIS MAGUFULI AFIKA KUWAPA POLE FAMILIA YA KIGWANGALLA

Rais Dkt. John Magufuli, leo ametoa mkono wa pole kwa familia ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye amefiwa na mwanae aitwaye Zul Hamis Kigwangalla jana Februari 21, 2019 Jijini Dar es Salaam.


Rais Magufuli akiwa na Mkewe, Mama Janeth Magufuli wamefika nyumbani kwa familia hiyo maeneo ya Vitoria, Mikocheni A, jijini Dar es Salaam na kuwapa pole baadhi ya wanafamilia wakiwamo Mama wa Marehemu, Dkt. Bayoum Kigwangalla waliokiwa katika maandalizi ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Nzega Mkoani Tabora kwa mazishi.

Rais Dkt. John Magufuli akiwapa pole na Dkt. Bayoum Kigwangala (Mke wa Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Kigwangala), pamoja na Bi Hawa Mushi na Bi. Bagaile Bakari nyumbani kwa Waziri huyo.

Aidha, baba wa marehemu, Dkt. Hamis Kigwangalla tayari ameshatangulia Nzega ambako mazishi yatafanyika baadaye leo jioni.

BREAKING: Ajali Mbaya Ilivyoua Watu 19, Majeruhi Wasimulia!

Comments are closed.