The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Akutana na Gwajima Ikulu – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John  Magufuli akisalimiana na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima  baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

RAIS John Magufuli amekutana na kuzungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Dkt. Josephat Gwajima leo Juni 3, 2019, Ikulu jijini Dar es Salaam.

…Wakiwa katika mazungumzo.

Akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, Gwajima amempongeza Magufuli kwa ujenzi wa mradi wa Stiegler’s Gorge akisema umeme wa mradi huo utakuwa mkubwa kuliko umeme wowote ambao Tanzania ilishawahi kuzalisha tangu uhuru, hivyo yatakuwa ni manufaa makubwa kwa taifa letu.

“Tuelewe ili ule chips yai lazima uvunje mayai, namshukuru rais kwa juhudi za Stiegler’s Gorge, tutakapozalisha umeme mwingi kuliko tuliozalisha zamani.  Kama unavyojua watu wengi wa Magharibi wanasema eneo hilo ni la mazingira lakini ukweli ni siasa tu.

 

 

 

Magufuli akiwa na ujumbe uliofuatana na Gwajima. Wengine ni Naibu Waziri Ofisi wa Waziri Mkuu Kazi, Vijana Ajira Anthony Mavunde (wa kwanza kushoto).      PICHA NA IKULU.

“Mwendo huu ni mchakamchaka si mwendo wa wazembe,” amesema Gwajima baada ya mazungumzo hayo. 

 

Hivi karibuni ilizuka taharuki kufuatia kusambaa kwa kipande cha video ambayo ilidaiwa kumwonesha mtu aliyefanana na Gwajima akishiriki mapenzi na msichana,  lakini Gwajima aliibuka na kukana akisema ni video ya kutengenezwa na watu wenye nia ovu ya kumchafua.

BREAKING: Askofu GWAJIMA Atinga IKULU “LAZIMA mayai YAVUNJIKE”

Comments are closed.