The House of Favourite Newspapers

RAIS MAGUFULI APOKEA NDEGE MPYA YA AIRBUS 220 – 300

Ndege mpya aina ya Airbus 220 – 300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikitua kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23,2018
Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali ikimwagiwa maji ikiwa ni ishara ya karibu na heshima (Water salute) kwa mara ya kwanza katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23,2018.
Viongozi na Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) wakiwapongeza na kuwakaribisha wenazao amabao walitoka safarai na Ndege mpya aina ya Airbus 220 – 300 ambayo imenunuliwa na Serikali mara ya kuwasili katika ardhi ya Tanzania Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,Balozi wa Canada Pamela O’donnel pamoja na viongozi wengine mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23,2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Ladislaus Matindi mara baada ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220-300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23,2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mmoja wa Marubani Kapteni Pandya aliyekuja na ndege hiyo mara baada ya kuwasili katika katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Leonard Chamuriho wakisaini mkataba wa makabidhiano ya Ndege mpya ya Airbus 220-300 itakayokabidhiwa katika shirika la ndege la Tanzania mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na viongozi wengine wakishuhudia kabla ya kuwasili kwa Ndege mpya aina ya Airbus 220 – 300 ambayo imenunuliwa na Serikali.Hafla iliyofanyika katika Uwanja ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Desemba 23,2018
Katibu mkuu kiongozi Balozi Dkt.John Kijazi pamoja na katibu mkuu wa Wizara ya Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi Dkt.Leonard Chamuriho wakionyesha mikataba mara baada ya kusaini mkataba wa makabidhiano ya Ndege mpya ya Airbus 220-300

Rais John Magufuli amesema viongozi wa Serikali waliokatiwa tiketi ili wasafiri na ndege za Shirika la ATCL na kukaidi watakatwa pesa hizo katika mishahara yao.

Ameyasema hayo leo Jumapili Desemba 23, 2018 wakati akipokea ndege mpya ya Airbus 220-300 ‘Dodoma’ katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya abiria wamekuwa wakikosa tiketi kwa kuambiwa ndege imejaa ila wanapoingia ndani hakuna watu huku baadhi ya tiketi zikiwa za watendaji wa Serikali ambao hawasafiri.

“Mtumishi anatakiwa kusafiri kwenye ndege na amekatiwa tiketi na Serikali lakini hasafiri na kufanya ndege iende tupu, nimeshamwambia mtendaji mkuu aniletee orodha ya watendaji ambao hawakusafiri tuwakate hizo hela kwenye mishahara yao,” amesema Rais Magufuli.

“Nimeambiwa wanakadiriwa kuwa 100 kwa hiyo nina uhakika kufika wiki ijayo nitapata majina yao, mawaziri, wabunge ambao walikaa hadi saa ya mwisho ndege ikaenda tupu na hela za Serikali zikaenda,” ameongeza Rais Magufuli huku akisema tena anafikiri kesho Jumatatu yatamfikia.

Amesema watumishi hao wajiandae kurudisha fedha hizo kutoka mifukoni mwao ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wanaotumia fedha za Serikali vibaya.

“Niwaombe tu watendaji kama kuna tiketi ambayo haukuitumia leta tu hela mara moja ili mambo yaishe lakini ni matumaini yangu sasa katika suala hili la tiketi ATCL mtajipanga vizuri,” amesema Magufuli.

 

 

Comments are closed.