The House of Favourite Newspapers

Magufuli Kuhutubia Bunge Ijumaa

0

 

RAISDk John Magufuli anatarajiwa kulihutubia Bunge la 12 Ijumaa Novemba 13, 2020,  saa 3:00 asubuhi, Dodoma,  kuashiria kuanza rasmi kwa Bunge.

 

Akizungumza bungeni jijini Dodoma mapema leo hii Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema desturi ya Bunge linapoanza mara baada ya kutoka katika uchaguzi kuna hotuba ya rais wa nchi kuhutubia Watanzania.

 

“Ninawataka Ijumaa saa tatu kamili asubuhi kuhudhuria tukio hilo bila kukosa kumsikiliza mheshimiwa rais atakachosema. Waheshimiwa wabunge najua mmewasili kwenye siku kadhaa sasa lakini baada ya kuapa tu hapa, sasa mambo yote tutarekebisha yanayohusiana na utaratibu. Pia natambua kuwa waheshimiwa wabunge mnao wageni wengi, mnayo mambo mengi ya kurekebisha hapa mjini.

 

“Wengine bado mambo ya makazi hayajakaa sawasawa, wengine simu za wajumbe bado nyingi sana…… Wajumbe bado wanafatilia, lazima upate muda wa kuwasiliana na wajumbe. Wabunge ni watu wenye shughuli nyingi sana kwa hiyo tumeona mchana wa leo tuwaachie muwe huru mrekebishe mambo yenu ili tuweze kukutana kesho saa tatu kwa shughuli za kesho kwa maana hiyo naahirisha shughuli za bunge mpaka kesho saa tatu,” amesema Ndugai.

 

Pia mapema Ndugai aliwakumbusha wabunge desturi ya bunge linapoanza baada ya kutoka kwenye uchaguzi, hotuba ya Rais kuhutubia bunge. Amewataka kuwahi mapema Ijumaa asubuhi kwa ajili ya kumsikiliza.

 

Leave A Reply