The House of Favourite Newspapers

Biden Kumpendekeza Obama Balozi Uingereza

0

VYOMBO vya habari vya Uingereza vimesema, kama Joe Biden akiapishwa kuwa rais, huenda atampendekeza rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama, kuwa balozi wa nchi hiyo nchini Uingereza.

 

Kutokana na hoja zisizo za kirafiki kuhusu rais huyo wa zamani zilizotolewa na waziri mkuu wa Uingereza Borris Johnson, uteuzi huo utaweza kuwa kikwazo kwa Boris kwa kuwa viongozi hao wawili walikuwa na mikwaruzano.

 

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza, ingawa matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu wa Marekani hayajatolewa, mgombea urais wa Chama cha Democrats, Joe Biden, anayeongoza katika uchaguzi huo ameanza kutekeleza mpango wa mpito ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi hiyo na kubadili sera kadhaa za serikali ya Trump.

 

Leave A Reply