The House of Favourite Newspapers

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI SHEREHE ZA MIAKA 50 YA BAKWATA – VIDEO

Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Maulid litakalofanyika wilayani Korogwe mkoani Tanga.

 

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi amesema leo, Jumanne Novemba 13, 2018,  kuwa baraza hilo limeandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) ambapo Maulid hayo ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yatafanyika Novemba 19.

 

Aidha, amewataka wananchi wa Tanga na mikoa jirani kuhakikisha wanafika kwenye maulidi hayo yanayofanyika mara moja kwa mwaka, huku akisema kuchaguliwa mkoa huo ni bahati hivyo wajitokeze kwa wingi.

 

Kiongozi huyo wa kiroho, amekemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili nchini akisema hatua hiyo ndiyo chanzo cha vijana wengi kupiga picha za utupu bila aibu na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii na kwamba vitendo hivyo vinavunja hadhi ya nchi na kuomba waliofanya hivyo wakadhibitika sheria kali zichukuliwe dhidi yao ili angalau kukomesha hali hiyo inayotia doa taifa kwa ujumla.

 

”Hii inasababishwa na malezi mabaya nyumbani kwani mtu mwenye akili timamu hawezi kuvunja heshima yake kwa kuweka picha chafu za kwenye mitandao ya kijamii huo ni uvunjifu wa maadili kwa kiasi kikubwa,” amesema

 

Alisema mengi yanayohusu kukemea tabia hiyo yataongelewa na watu maalum kwenye maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa baraza hilo hapa nchini ambalo lilianzishwa mwaka 1968 mpaka sasa.

 

MIAKA 50 YA BAKWATA: Mufti mkuu atangaza Maulid

Comments are closed.