The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli: Ole Wenu… Mtazitapika Hizo Bilioni 3.7 – (Video)

Rais Dkt. John Magufuli amesema atalipa mishahara ya wafanyakazi wa Marine Service kiasi cha Ths. Bilioni 3.7 wanazoidai serikali ndani ya wiki mbili ili wafanye kazi kwa nguvu kujituma na kuzalisha zaidi na wakishindwa kuzalisha ‘watazitapika’.

 

Magufuli ameyasema hayo leo Septemba 03, 2018 wakati akishuhudia utiaji saini wa mkataba wenye thamani ya Shilingi bilioni 152 kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya, ukarabati wa meli za MV Victoria na MV. Bitiama na ujenzi chelezo katika ziwa Victoria, tukio hili lilofanyika Jijini Mwanza.

 

“Wakati ninaahidi kujenga meli mpya Ziwa Victoria nilikuwa sijui kama itawezekana, nilijiuliza hivi kuna nini huko mbona wenzangu wameshindwa kwa miaka 22 tangu MV. Victoria ilipozama? Tulipotangaza tenda ya kujenga meli mpya Ziwa Victoria, kumpata mkandarasi ilikuwa kazi sana.

“Lakini nchi inayoongoza kwa kuunda meli ni Korea. Nikaona tujifunze kutoka kwao, nikamchagua Balozi atakayetuwakiliasha Korea harakaharaka ili kukuza ushirikiano.

“Wafanyakazi wa Marine Service nitawalipa Ths. Bilioni 3.7 ndani ya wiki mbili lakini na nyinyi mjirekebishe, mkishindwa mtazitapika. Tiketi za elekroniki zitumike badala ya zile za enzi za ujima, mafuta yafanyiwe evaluation.

“Hizi meli nimezipanda sana nikiwa nakwenda Nyamirembe, kulikuwa na kamchezo wafanyakazi walikuwa wanaiba mafuta wanauza, walikuwa wanatoa hata tiketi hewa, kulikuwa na mama mmoja hapa alifanya ya hovyo, najua.

“Wafanyakazi wa Marine Service mbadilike, haiwezekani mna meli 14 mnakosa mishahara, wakati wenye mitumbwi wanatengeneza pesa na wanapata, ina maana wana akili kuliko nyinyi? Mnatakiwa mfanye biashara. Ninawapa muda wa kujirekebisha,” alisema Magufuli.

Rais Magufuli: Ole Wenu… Mtazitapika Hizo Bilioni 3.7 – Video

Comments are closed.