The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli: Yeyote Atakayethubutu Kuuvunja Muungano wa Tanzania, Atavunjika Yeye (VIDEO)

1

DODOMA: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa onyo kuwa, yeyote atakayejitokeza na kuthubutu kufanya jambo lolote la kuuvunja Muungano wa Tanzania basi atavunjika yeye.

Rais ameyasema hayo leo katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma wakati akitoa hotuba yake kwenye Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Aidha Rais Magufuli amewataka Watanzania wote kuulinda kwa nguvu zote na kuudumisha muungano huo pamoja na kudumisha yale yaliyoasisiwa na Waanzilishi wa Taifa leu ambao ni Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyere na Mzee Abeid Aman Karume.

1 Comment
  1. […] Twitter0 […]

Leave A Reply