The House of Favourite Newspapers

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki katika Tamasha la Vyakula vya Baharini (Zanzibar Seafood Festival)

0

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki katika Tamasha la Vyakula vya Baharini (Zanzibar Seafood Festival) Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.

Rais Samia akitembelea baadhi ya Mabanda

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika Fukwe za Kendwa ametembelea mabanda mbalimbali ya Maonesho ya Biashara kwenye msimu wa pili wa Tamasha la Vyakula vya Baharini (Zanzibar Seafood Festival 2023) lililofanyika katika ufukwe hizo zilizopo Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.

 

Mara baada ya kutembelea Mabanda hayo ya Maonesho, Mhe. Rais Samia amewapongeza Vijana wa Skydivers kwa kuendelea kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo nchini hususani katika uwekazaji. Vijana waliruka kwenye Ndege umbali wa mita 10,000 huku wakiwa na Bendera ya Tanzania yenye ujumbe wa Wekeza Tanzania Invest Tanzania.

 

Pia katika Tamasha hilo Mhe. Rais Samia amekabidhi  Boti 40 za Uvuvi kwa ajili ya vikundi mbalimbali vya Uvuvi wa Samaki na mazao Bahari kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye msimu wa pili wa Tamasha la Vyakula vya Baharini (Zanzibar Seafood Festival 2023) lililofanyika katika ufukwe wa Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar.

Rais Samia akikabidhi boti kwa vikundi vya uvuvi

 

Mara baada ya kukabidhi Boti hizo, Mhe Rais amewaasa wafaidika wa boti hizo kufanya kazi kwa bidii na kwamba Serikali itazifatilia kwa muda wote ili ziweze kukidhi matarajio yaliyowekwa.

Leave A Reply