The House of Favourite Newspapers

Mnangagwa Aruhusu Wajawazito Kuendelea na Masomo

0

RAIS wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, amesaini sheria inayozuia shule za serikali kuwatenga wasichana ambao ni wajawazito kuhudhuria masomo.

 

Chini ya marekebisho hayo ya sheria, walimu pia hawaruhusiwi tena kuwachapa viboko wanafunzi. Sheria mpya pia inasema kwamba hakuna mwanafunzi atakayetengwa shuleni kwa kutokulipa karo ya shule.

 

Kabla ya marekebisho ya sheria, viongozi wa shule walikuwa na uwezo wa kumfukuza msichana kwa kupata ujauzito lakini kumwacha mvulana anayehusika na ujauzito huo. Kitendo hicho kilionekana kama ubaguzi dhidi ya mtoto wa kike.

 

Wasomi na wadau wa elimu wameyakaribisha marekebisho hayo na kuyataja kuwa ni maendeleo makubwa. Naye Waziri wa Elimu ya Msingi na Sekondari Kaini Mathema alisema amefurahi kwamba rais amesaini sheria hiyo mpya.

 

CREDIT: www.newzimbabwe.com

Leave A Reply