The House of Favourite Newspapers

Haitham Akiri Kuishi kwa Kudanga, Asimulia Mazito!

0

HAITHAM Kim ni moja kati ya wasanii wanaokuja kwa kasi kunako anga la Bongo Fleva, amefanya vizuri kupitia ngoma zake kama Ananichora, Yaishe na Nionyeshe.

 

Risasi Jumamosi limezungumza naye, ambapo pamoja na mambo mengine, amezungumzia suala la yeye kujihusisha na uuzaji wa mwili wake (kudanga), karibu:

Risasi: Kwanza kabisa wasomaji wangependa kujua umejaaliwa watoto wangapi?

Haitham: Nina watoto wawili wa kike.

 

Risasi: Muonekano wako mtu akikutazama, utadhani haujazaa kabisa, nini siri ya urembo wako?

Haitham: Siri kubwa ya kwanza ni kujitunza, na mimi ni msichana ambaye niliweza kujitunza kabla sijaingia kwenye maisha ya ndoa na hata maisha ya kuwa mama.

Ukijichezea kwa kubadilisha wanaume hovyo, thamani yako itashuka na hata viungo vyako vya mwili pia vitalegea.

 

Risasi: Wanawake wengi wakishatoka kujifungua, huwa hawanyonyeshi watoto wao kwa muda unaotakiwa, wengi wao huwa wana waachisha mapema kunyonya kwa kuogopa maziwa yao kulala, lakini wewe naona kifua chako bado kipo imara (hakijalala) vipi na wewe ulinyonyesha watoto wako kwa muda mfupi?

Haitham: Ndiyo nimenyonyesha, lakini hawakunyonya kwa muda mrefu, kwa sababu kawaida inatakiwa mama amnyonyeshe mtoto kwa muda wa miaka miwili, lakini mimi wanangu wote walinyonya mwaka mmoja mmoja.

 

Risasi: Huwa unavaa sidiria?

Haitham: Hapana sivai, kwa sababu sisi kwetu asili yetu huwa maziwa hayalali hata tunyonyeshe vipi.

Risasi: Mmmh! Sio kwamba umetumia dawa ya kusimamisha matiti?

Haitham: (Anacheka) Hapana sijatumia dawa, ni umbile tu.

 

Risasi: Una muda gani kwenye ndoa yako?

Haitham: Nina miaka miwili na niliolewa nikiwa na miaka 24, hivyo sasa nina miaka 26.

Risasi: Asilimia kubwa ya mabinti wa siku hizi, huwa hawapendi kuolewa mapema, kwa nini wewe uliamua kuwahi kuingia kwenye ndoa?

 

Haitham: Ni kweli wasichana wengi siku hizi wanataka kumaliza kwanza starehe, lakini binafsi sikutaka mwanaume anichezee, nilipomuona ana malengo na nia ya kuwa na mimi, nikamuuliza kama  yupo tayari kuishi na mimi, akaniambia ndiyo, basi tukaenda kwa wazazi, mwisho wa siku tukaoana.

Risasi: Unawashauri nini mastaa wa kike ambao wanaingia kwenye ndoa, kisha baada ya miezi au mwaka mmoja, wanaachana?

 

Haitham: Nawashauri wakiwa kwa waume zao, wasilete usupastaa, kuwa kama mke, pia mheshimu mume wako usijifanye eti kwa sababu ni staa, basi ukiitwa au kutumwa kitu usiende, hapana hatuishi hivyo. Mpende, mheshimu, mjali na msikilize mumeo, utadumu kwenye ndoa yako.

Risasi: Kuna jambo lolote baya limewahi kukutokea kwenye uhusiano wako, mpaka ukafikia hatua ya kujuta kuwahi kuingia kwenye ndoa?

 

Haitham: Kiukweli sijawahi kujuta, lakini siku zote matatizo hayakosekani kwenye ndoa, na siku zote ndoa rafiki yake ni mvumilivu, hivyo kuna wakati unakuta unakwazika, unakasirika, lakini ni mambo ya kawaida, mwisho wa siku tunayamaliza wenyewe.

Risasi: Wewe ni mrembo halafu mdogo, mbali na yote una kipaji kizuri cha kuimba, vipi hausumbuliwi na wanaume wakware mtandaoni?

 

Haitham: Nasumbuliwa sana, kwa siku natakiwa na wanaume wengi mno, tena na mastaa wakubwa na wengine ni mashabiki zangu, lakini siwezi kuwakubalia kwa sababu mimi tayari ni mke halali wa mtu.

Risasi: Mumeo analijua hilo?

Haitham: Ndiyo anajua kwa sababu kwanza yeye ndiyo mtu ambaye ‘ana-control’ platform zote za mitandao yangu, lakini siyo mtu wa wivu kwa sababu anajua ninajiheshimu.

 

Risasi: Tunafahamu mume wako anafanya kazi ya kuchora tattoo, vipi hauoni wivu? Maana kuna muda anawachora tattoo wanawake warembo na wazuri kukuzidi, tena sehemu za uchokozi.

Haitham: Kuna muda kweli nakuwa na wivu, unashangaa mdada kajaaliwa shepu nzuri na sura, anaenda pale anataka achorwe tattoo kiunoni, naumia lakini navumilia. Sasa nitafanyaje na ndiyo kazi inayotuingizia kipato.

 

Risasi: Una tattoo ngapi kwenye mwili wako?

Haitham: Nina tattoo zaidi ya kumi.

Risasi: Inasemekana kuwa tattoo zinauma sana, kwa nini umeamua kuchora zote hizo na wewe ni mtoto wa kike?

Haitham: Zinauma lakini maumivu yake unaweza ukavumilia.

 

Risasi: Na tattoo zote ulizochora, zina maana gani?

Haitham: Kila tattoo ina maana yake, mfano kama hii ya mguuni nimeandika tarehe na mwezi wa kuzaliwa mume wangu, kuna nyingine ipo mgongoni nimeandika ‘God is my judge’ (Mungu ndio hakimu wangu) halafu na nyingine zilizobaki nazo zina maana yake.

 

Risasi: Vipi kuhusu wazazi wako, nao umewachora tattoo?

Haitham: Ipo ya baba yangu nimeandika Dady, lakini mama yangu yeye siyo mpenzi wa hivi vitu na alishawahi kunionya kuwa nisimuweke kwenye mwili wake, sasa unajua mzazi akishakuonya usilazimishe, na kiukweli nampenda sana mama yangu, hivyo akibaki moyoni mwangu inatosha.

 

Risasi: Umeshawahi kudanga?

Haitham: Ndiyo, nimeshawahi kudanga kabla sijaolewa.

Risasi: Changamoto gani ambazo ulizipitia kipindi unadanga?

 

Haitham: Yaani unakuta unaenda na mtu mnakubaliana kiasi fl’ani, ikifika asubuhi kakukimbia au anakuambia ngoja niende Bank nakurudia, lakini harudi, jambo lingine unaweza ukakopwa na usilipwe. Kwa hiyo, hayo mambo yapo na nilikuwa napitia wakati mgumu sana.

Risasi: Umesema sasa hivi umeacha kwa sababu ya ndoa, labda umeshawahi kukaa na kujutia kwa nini ulikuwa unafanya hayo yote kabla haujaolewa?

 

Haitham: Ndiyo, kuna muda nikikaa, huwa najuta kwa nini nilikuwa natumia mwili wangu kujipatia pesa, halafu hii dunia ni ndogo, unaweza ukapita sehemu unakutana na mtu ambaye umeshawahi kumdangia halafu unaanza kuona aibu.

Lakini naamini nilipitia hayo yote kwa sababu Mungu alikuwa anataka kunikutanisha na mwanaume bora wa maisha yangu.

 

Risasi: Unawazungumziaje wanawake ambao wanaendesha maisha yao kwa kudanga?

Haitham: Kudanga sio kitu kizuri na itafikia hatua wataacha, lakini mimi naamini mpaka mtu ameamua kudanga, kuna sababu anapitia, mwingine unakuta ana maisha mazuri tu lakini ameamua kufanya hivyo kwa sababu anaipenda hiyo starehe.

 

Lakini mwingine unakuta hapendi ile starehe, ila anafanya tu kwa sababu ana maisha magumu, kwa hiyo kila mtu ana tabia zake za kufanya hivyo.

Risasi: Umesema una watoto wa kike, jambo gani ambalo umewahi kulipitia na hautamani na wao waje wapitie?

 

Haitham: Nimewahi kupitia vitu vingi sana; kudharauliwa, kutumika kama chombo cha starehe, hivyo natamani wanangu wasipitie haya.

Risasi: Una jambo gani la mwisho kwa mashabiki zako?

Haitham: Nawashukuru sana kwa sapoti yao.

Makala: Memorise Richard

Leave A Reply