The House of Favourite Newspapers

Rais Mstaafu Kikwete Ashinda Tuzo Ya Kiongozi Wa Amani Na Usalama Wa Mwaka 2023 Ya Jarida La Uongozi Wa Afrika

0
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa Mwenyekiti wa Jarida la Uongozi Afrika, Dk. Ken Giami kwenye hafla ya kila mwaka ya Tuzo za Watu Bora wa Mwaka za ALM katika Hoteli ya Ethiopian Skylight jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais William Ruto wa Kenya, na Rais wa zamani wa Liberia George Weah wameibuka Kuwa washindi katika tuzo za 12 Viongozi Bora wa Mwaka wa Jarida la Uongozi wa Kiafrika kwa mwaka wa 2023.

Watatu hao wameshinda katika vipengele vya Kiongozi wa Usalama wa Mwaka, Mwafrika wa Mwaka, na Kiongozi wa Kisiasa wa Mwaka, mtawalia, kulingana na matokeo ya kura ya mtandaoni ambayo iliona ongezeko la asilimia 29 kwa kura ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Tuzo za Watu Bora wa Mwaka za ALM, zinazotambulika kama tuzo kuu za viongozi bora barani Afrika, zinaenzi viongozi ambao wanachangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya bara hilo, kubadilisha hadhi yake, na kukuza maendeleo chanya.

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa na Waziri wa Mapato wa Jamhuri ya Ethiopia, Mama Aynalem Nigusie) Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Innocent Shiyo.

Mwenyekiti wa Jarida la Uongozi Afrika, Dk. Ken Giami, amesisitiza hatua kubwa na michango ya washindi katika Uhai wa Mwamko wa bara la Afrika katika kuendesha maendeleo endelevu, ukuaji wa kiuchumi, na utulivu wa kisiasa.

“Juhudi zao zimeimarisha amani kikanda, zimeboresha huduma za afya na elimu, na zimeunda msingi imara wa utajiri wa kiuchumi na maendeleo ya rasilimali watu katika Afrika,” alisema.

Sherehe rasmi za kutunuku tuzo hizo zimefanyika jioni ya tarehe 15 Machi, Mwaka 2024 kwenye hafla ya kila mwaka ya Tuzo za Watu Bora wa Mwaka za ALM katika Hoteli ya Ethiopian Skylight huko Addis Ababa, Ethiopia, makao makuu ya Umoja wa Afrika.

Rais Mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na tuzo.

Sherehe hizo zilizoandaliwa na ALM kwa ushirikiano na Tume ya Forodha ya Ethiopia, zimeshuhudia kuzinduliwa kwa toleo maalum la POTY la Jarida la Uongozi la Afrika, Daftari la Mwaka la Wakuu wa Forodha na Bandari wa Afrika kwa mwaka 2024.

Dkt. Kikwete alikabidhiwa tuzo yake na mgeni rasmi, Waziri wa Mapato wa Jamhuri ya Ethiopia, Mama Aynalem
Nigusie) na Mwenyekiti wa Jarida la Uongozi Afrika, Dk. Ken Giami.

Akipokea tuzo hiyo, Rais Mstaafu amewashukuru waandaaji wa tuzo hizo na waafrika kwa ujumla na amesema tuzo hiyo ni kwa ajili ya Waafrika wote; viongozi wa kisiasa, wana mageuzi ya kiuchumi, viongozi wa dini, Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Watumishi wa Umma wanaojitoa kwa dhati, wakulima, wafugaji na wananchi wa kawaida wote – ambao wanaamka kila siku kupambania Bara la Afrika kuwa sehemu bora ya kuishi.

RAIS MAGUFULI ALIVYOKATAA DHAMBI ya KUWANYONGA WAFUNGWA 78 – ”WATUMIKE SANA” | VIDEO YA MAKTABA

Leave A Reply