Rais Mstaafu Kikwete Azindua Mpango Wa Kuanzisha Huduma Harakishi Za Watoto Wachanga
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amezindua Mpango Harakishi wa Kuanzisha Huduma za Watoto Njiti na Watoto Wachanga Tanzania katika siku ya mwisho ya Mkutano wa Pili wa Kisayanzi ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto uliofanyika kwa siku tatu kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.