The House of Favourite Newspapers

Rais Mwinyi Afanya Uteuzi Wizara ya Afya

0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi, leo Septemba 8, 2021 amefanya uteuzi wa wakurugenzi sita wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mhandisi Zena Said, walioteuliwa ni Dkt. Amour Suleiman Mohamed anayekuwa  Mkurugenzi wa Tiba na Dkt. Ali Said Nyanga anayekuwa Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya.

 

Wengine ni Dhameera Mohamed Khatib aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti, Mwantoum Ramadhan Mussa aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Uendeshaji, Abduylla Saleh Omar aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ustawi wa Jamii na Wazee na Salim Slim Tawakal aliyeteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya.

Leave A Reply