The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya Uteuzi na Uhamisho wa Watendaji wa Serikali

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt.Charles Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI (Elimu), Bw.Msonde anachukua nafasi ya Gerald Mweli ambaye amehamishiwa Wizara ya Kilimo.

Kabla ya uteuzi huu Dkt.Msonde alikuwa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Pia, Rais Samia amemteua Dkt. Maduhu Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani akichukua nafasi ya Ramadhan Kailima aliyehamishiwa TAMISEMI

Leave A Reply