The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Alivyowasili Mkoani Arusha Asubuhi ya leo

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili mkoani Arusha asubuhi ya leo na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda, pamoja na Viongozi wa Chama na Serikali,wakiambatana na Kamati za Usalama za mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, leo tarehe 12 Aprili, 2024.

Rais amewasili mkoani Arusha kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro, akielekea wilaya ya Monduli kushiriki Ibada Maalum ya Kumbukumbu ya Miaka 40 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza, Hayati Edward Moringe Sokoine

Ibada hiyo itakayofanyika nyumbani kwake kijiji cha Enguik, kata ya Monduli Juu, wilaya ya Monduli, itaongozwa na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha, Askofu Issac Aman tarehe 12 Aprili, 2024

Leave A Reply