The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awasili Kenya Kushuhudia Ruto Akiapishwa Kuwa Rais (Picha +Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe ya kuapishwa kwa Rais Mteule wa Kenya William Samoei Ruto tarehe 13 Septemba, 2022.

RAIS wa Tanzania Samia Suluhu leo Septemba 13, 2022 amehudhuria sherehe kuapishwa kwa Rais Mteule wa Kenya William Samoei Ruto.

Rais Samia ameambatana na baadhi ya Viongozi wa Serikali akiwemo Balozi Liberata Mulamula, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Dkt. Ashatu Kijaji, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Harusi Said Suleiman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Leave A Reply