The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Amlipua Diwani Mkorofi Kigamboni – Video

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemlipua diwani wa Kigamboni ambaye amedai kuwa amekuwa kikwazo kikubwa kwa kuwarubuni wananchi kugomea miradi na maelekezo ya Serikali.

 

Mhe. Samia amesema hayo leo Disemba 13, 2021 wakati wa akishuhudia utiaji saini ya Makubaliano kati ya Serikali na Kampuni za Uchimbaji Madini za Black Rock Mining Limited, Strandline Resources Limited na Nyanzaga katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam.

 

“Kazi ya kusimamia utoroshaji wa madini haiwezi kufanywa na vyombo pekee vya ulinzi na usalama, ni pamoja na wananchi wenyewe. Kila mmoja asimamie na hatutaruhusu hili kutokea. Tuongeze nguvu kuthibiti utoroshaji wa madini.

 

“Miradi hii ni muhimu kushirikisha wananchi. Wasipokuwa na uelewa ndiko kunatokea ukorofi. Mpango wa kuchimba mchanga Kigamboni wananchi wa Kigamboni hawapo hapa wakati wa kutambulisha mradi sababu wameshaanza vurugu wakiongozwa na diwani wao.

 

“Diwani huyohuyo wa Kigamboni ndiye pekee aliyepinga wamachinga kuhamishwa, sijui ana shida gani, na wakati wa mradi wa kuchimba mchanga ameongoza wananchi wa Kigamboni kufanya vurugu, tuwaeleweshe waelewe umuhimu wa mradi huu, wataulinda na kuuthamini.

 

“Niwakumbushe wawekezaji kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo inayosimamia sekta hii ikiwemo ushirikishwaji wa Watanzania kwenye fursa mbalimbali za ajira na utoaji huduma.

 

“Fadhira kwa wananchi nalo ni muhimu. Kama tunakwenda kuchimba (madini) na kuondoka, turudishe fadhira kwao kwani eneo hilo tunalochuma mali ni la kwao. Wabunge msiende kufaidika wenyewe,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply