The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Moto wa Magufuli Sitauzima – Video

0

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema moto wa kusimamia rasilimali za taifa yakiwemo madini uliowashwa na mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli hatouzima, badala yake atauendeleza ili Taifa linufaike na rasilimali zake.

 

Mhe. Samia amesema hayo leo Disemba 13, 2021 wakati wa akishuhudia utiaji saini ya Makubaliano kati ya Serikali na Kampuni za Uchimbaji Madini za Black Rock Mining Limited, Strandline Resources Limited na Nyanzaga katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam.

 

“Kipindi cha nyuma tulisikia tu makampuni yanachimba madini katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, tena kwenye sauti za wananchi wakilalamika kuhusu uharibifu wa mazingira na vyanzo vya mwaji, hatukujua vizuri nini kinafanyika huko wala kinachochimbwa kinakwenda wapi.

 

“Tulikuwa tunasikia madini huku yamepenya, kule yamepenya, mara kwenye viwanja vya ndege. Niwaombe waliotumwa kusimamia utoroshaji wa madini, wajirudi na kulinda rasilimali zetu. Leo tunashiriki kama wabia kwenye uchimbaji wa rasilimali zetu muhimu na adhimu (mkadini) kwa ajili ya kuliletea maendeleo Taifa letu. Tunapaswa kujipongeza kwa hatua hii.

 

“Hatua ya safari hii sikuianza mimi, aliianza mwenzetu Dkt John Pombe Magufuli ambaye Mungu alimpa maono na ujasiri akasema hapana, rasilimali zetu sasa imefika wakati zifaidishe wananchi. Niwaombe kila mmoja wetu amuombee kwa Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

 

“Moto wa madini aliouwasha Dkt. John Pombe Magufuli nimeupokea, na ninaahidi hautazimika nitakwenda nao,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply