The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aongoza kupokea Mwili wa Rais Mstaafu Hayati Mzee Mwinyi Zanzibar

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na kumfariji Mama Siti Mwinyi, Mjane wa Rais Mstaafu awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar tarehe 01 Machi 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan aongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar kupokea Mwili wa Rais Mstaafu awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakiomba Dua mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi lilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar tarehe 01 Machi 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakishika Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi lilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar tarehe 01 Machi 2024.
Gari la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lililobeba Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi lilipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar tarehe 01 Machi 2024.
Leave A Reply