The House of Favourite Newspapers

Rais wa Zimbabwe Aahirisha safari yake Kwasababu ya Usalama

0

Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa ameahirisha safari yake Ijumaa hii baada ya kuripotiwa usalama mdogo katika Uwanja wa Ndege wa Victoria Falls.

Kwa mjibu wa Msemaji wa Rais, George Charamba alikiri kupokea ujumbe wa barua pepe (email) kuhusiana na kutegwa kwa bomu kwenye uwanja huo.

Hata hivyo baadae shughuli ziliendelea kama kawaida baada ya ukaguzi kufanyika katika Uwanja huo ambao Rais alikuwa anataka kuutumia kuelekea katika mkutano wa Kimataifa.

Victoria Falls ni miongoni mwa miji inayokaliwa na watalii wengi ukiwa Kilometa 900 kutoka mji Harare ulipokuwa unataka kufanyikia mkutano huo.

Leave A Reply