The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Apokea na kuridhia barua ya kujiuzulu ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo

0
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amepokea na kuridhia barua ya kujiuzulu ya Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.

Katibu wa NEC-Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, na ameridhia ombi hilo.

Kikao hicho pia kimejadili hali ya kisiasa ndani na nje ya Chama huku pia kikifanya uteuzi wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa (Arusha, Mbeya na Mwanza) na Wilaya (Mpanda na Kusini Unguja) ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.

Leave A Reply