The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Atoa Maagizo Wizara ya Fedha

0

Rais Samia Suluhu ameitaka Wizara ya Fedha na Mipango kufanya uratibu ujulikanao kama ‘Municipal Investment Financing’ ili kusaidia upatikanaji wa fedha kwa Serikali za Mitaa kupitia uanzishwaji wa hati fungani.

 

Rais Samia amesema hayo jana Oktoba 25, 2021 alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF), Preeti Sinha, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

 

Aidha, Katibu Mtendaji wa UNCDF, Preeti Sinha amemuahidi Rais Samia kuwa UNCDF ipo tayari kushirikiana Tanzania kutafuta njia za kupata fedha za kugharamia miradi ya maendeleo.

 

Amesema fedha zitakazopatikana kupitia hati fungani zitarejeshwa kutokana na makusanyo yanayopatikana kwenye Serikali za Mitaa. Rais Samia ameafikiana na wazo hilo kwa kuongeza kuwa litasaidia kupunguza mzigo kwa Serikali Kuu kuhudumia miradi ya maendeleo ya Serikali za Mitaa.

Leave A Reply