The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Atoa Pole Kwa Spika wa Bunge Kufuatia Kifo Cha Mbunge Irene Ndyamkama

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa Spika wa Bunge, Tulia Ackson Familia, Wabunge na Wananchi wa Mkoa wa Rukwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum, Irene Ndyamkama aliyefariki dunia leo katika hospitali ya Tumbi Mkoani Pwani.

 

“Natuma salamu za pole kwa Spika Mhe.@TuliaAckson Familia, Wabunge na Wananchi wa Mkoa wa Rukwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Irene Ndyamkama aliyefariki dunia leo katika hospitali ya Tumbi Mkoani Pwani. Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Amina” amesema Rais Samia.
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Irene Ndyamkama aliyefariki dunia leo katika hospitali ya Tumbi Mkoani Pwani.

Leave A Reply