Rais Samia Atunukiwa Udaktari Wa Heshima, kutoka Chuo Kikuu cha Ankara, Uturuki

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameshiriki hafla ya kutunukiwa Udaktari wa Heshima kutoka Chuo Kikuu cha Ankara, Uturuki, kutambua jitihada zake za kuendeleza mageuzi ya kijamii, kisiasa na kiuchumi -4R. Rais Samia yupo nchini humo kwa ziara rasmi aliyoianza tarehe 17 Aprili, 2024.





