The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awasili Cairo – Video

0

Rais Samia Suluhu Hassan, leo Novemba 10, 2021 amewasili jijini Cairo, Misri na kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu kwa mwaliko wa rais wan chi hiyo, Abdel Fattah Al-Sis.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Rais Samia amepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Cairo na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Uhamiaji na Wamisri walishio nje, Nabila Makram.

Baada ya kuwasili jijini Cairo, Rais Samia amefanya mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Al Sis ambapo wamejadiliana kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo ushirikiano kwenye nyanja za elimu, nishati, michezo, ulinzi na ushirikiano wa kijeshi ambapo pia Rais Samia amezungumza na waandishi wa habari.

 

 

 

Leave A Reply