Rais Samia Azindua Vizimba vya Kufugia Samaki, Agawa Boti Mwanza
Muonekano wa Boti za Kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amezindua ugawaji wake kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla iliyofanyika Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.
Boti na vizimba hivyo vimegaiwa kwa Wavuvi kwa mkopo usio na riba ili kuwawezesha kufanya Biashara ya Samaki kwa tija.