The House of Favourite Newspapers

Tamasha Kubwa La Utulivu Laja, Wasanii Wa Kizazi Kipya, Gospo Na Zilipendwa Kunogesha

0
Rais wa Taasisi ya Utulivu Experience, Ibrahim Regerera alipokuwa akizungumza na wanahabari kuhusiana na tamasha hilo kwenye Hoteli ya Hayatt Regecy The Kilimanjaro Hotel, leo.

Dar es Salaam, 30 Januari 2024: Taasisi ya Utulivu Space au Utulivu Experience imeandaa tamasha kubwa la Utulivu linalotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa The Super Dome uliopo Masaki jijini Dar, Aprili 20 mwaka huu, ambapo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, gospo na zilipendwa wanatarajiwa kunogesha tamasha hilo.

Rais wa Taasisi ya Utulivu Experience, Ibrahim Regerera akielekeza jambo kwenye mkutano na wanahabari, kushoto kwake ni Dk. Mboni Kibelloh na Jacob Mbuya na kulia kwake ni Mc Thom Luvanda ambao wote kwa pamoja ni waratibu wa tamasha hilo.

Akizungumza na wanahabari jijini leo, Rais wa Taasisi hiyo, Ibrahim Regerera amesema lengo la tamasha hilo ni kuitangazia dunia amani na utulivu wetu ambao tunajivunia na kuwakaribisha wote ulimwenguni kuja kuwekeza hapa nchini.

Regerera amesema katika tamasha hilo wataalikwa watu mbalimbali waliochangia kwa kiasi kikubwa amani na utulivu tulionao bila kuwasahau waliotangulia mbele za haki akiwemo Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na marais wetu wengine walioaga dunia na waliopo. HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL 

Leave A Reply