The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Hakuna Mwenye Misuli Na Ubavu Wa Kuligawa Taifa -Video

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) pamoja na Waumini wa Kanisa hilo, kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023

Amesema “Nimesikia kuhusu Usalama, Amani, Umoja na Muendelezo wa Taifa letu, niliamua kunyamaza na ninaendelea kuwa kimya. Ninachotaka kuwahakikishia ni kuwa hakuna mwenye Misuli na Ubavu wa kuligawa wala kuuza Taifa hili.”
Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika Chuo cha Tumaini Makumira Mkoani Arusha, Agosti 21, 2023
Aidha amesisitiza Serikali inawategemea Viongozi wa Kiroho katika kukuza na kusimamia maadili na Desturi za Nchi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mara baada ya kuzungumza nao kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa hilo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023

 

Leave A Reply