The House of Favourite Newspapers

Hafidh Konkoni Ashusha Presha ya Mabao Yanga, Azungumza na Championi

0
Hafidh Konkoni

MSHAMBULIAJI wa Yanga raia wa Ghana, Hafidh Konkoni amewaondoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo, kwa kutamka sasa hivi yupo fiti na tayari kuifungia mabao timu yake.
Konkoni ni kati ya washambuliaji wanaotegemewa katika kikosi  cha timu hiyo, ambaye aliletwa kuchukua nafasi ya Fiston Mayele.

Nyota huyo akiwa na Yanga amecheza mechi moja pekee ya mashindano akitokea benchi katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Konkoni alisema kuwa kwa muda ambao amekaa kambini Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam unatosha kwake kuwapa furaha kwa
kufunga mabao.

Konkoni alisema kuwa tayari ameshazoeana na wachezaji wake kwa sasa ambao amewakuta Yanga katika msimu huu, hivyo mashabiki watarajie makubwa katika michezo ijayo.

Aliongeza kuwa mashabiki wanatakiwa kutengeneza imani na yeye kwa sasa, kwani anafahamu kilichomleta Yanga.
“Sitakiwi kufananishwa na mchezaji yeyote ndani au nje ya Yanga, kikubwa nimepanga kufanya kile ambacho kimenileta hapa nilipo ambacho ni kufunga mabao pekee.
“Hadi sasa bado sijafanya kile ambacho ninataka kukifanya, sasa basi huu ni wakati wangu
muafaka wa mimi kufunga baada ya kuwa tayari na fiti kucheza mechi.
“Haitakuwa rahisi kwangu kufanya kitu kikubwa bila ya sapoti kubwa ya mashabiki ambao wanatakiwa kuniamini,” alisema Konkoni.

STORI NA WILBERT MOLANDI, CHAMPIONI JUMATATU

BANGWE FC YATINGA NUSU FAINALI KIABABE SHIGONGO CUP YAICHAPA BULYAHEKE (1-0)

Leave A Reply