The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Kufanya Ziara ya Siku 2 Arusha

0

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hasani anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi siku mbili mkoani Arusha, ambapo atazindua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

 

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, leo Alhamisi Oktoba 14, 2021 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amesema Rais atawasili mkoani humo Oktoba 16.

 

Amesema akiwa mkoani humo, atatembelea mradi wa maji wenye thamani ya Sh520 bilioni uliopo Chekereni wilaya ya Arumeru, pamoja na kuzindua mradi wa Hospitali ya Wilaya iliyopo Engutoto unaojengwa na fedha za ndani za Halmashauri ya jiji la Arusha.

 

“Baada ya uzinduzi huo Rais Samia anatarajia kuhutubia wananchi katika Uwanja wa Mpira wa Sheikh Amri Abeid” amesema.

 

Mongela amesema Oktoba 18, Rais atazindua Kiwanda cha Nyama Elia Food Overseas LTD kilichopo Namanga wilayani Longido, atazindua mradi wa maji wilayani hapo pamoja na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

 

Leave A Reply