The House of Favourite Newspapers

Rais Samia, Museveni Wazindua Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo (Picha + Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.
Rais Samia akivuta kamba pamoja na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023. Mradi huo wa umeme utanufaisha nchi zote mbili katika masuala ya Nishati ya umeme.
Rais Samia akizungumza na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati alipotembelea mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo (Megawatt 16), Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.
Eneo la mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo pamoja na Mitambo kama linavyoonekana pichani, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati wakisikiliza maelezo ya mradi wa kufua umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda tarehe 25 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan leo Mei 25, 2023 amezindua Mradi wa Umeme wa Kikagati – Murongo, Mbarara nchini Uganda akiwa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Leave A Reply